Ushiriki wa mwanamke katika kulinda, kutunza mazingira
16 April 2024, 10:21 am
Wakati mkutano wa 23 wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, COP 23, ukiingia wiki ya mwisho ya majadiliano mjini Bonn, Ujerumani, Rais wa mkutano huo alitangaza mpango wa utekelezaji wa kijinsia kwa kutambua nafasi ya wanawake katika suala la mabadiliko ya tabianchi.
Na Mariam Kasawa.
Utunzaji wa mazingira unatajwa kumgusa mwanamke moja kwa moja kwa kuwa shughuli zake za kila siku zina uhusiano wa karibu na mazingira.
Wanawake wana mchango mkubwa sana katika uhifadhi wa mazingira kwa kuwa shughuli nyingi za nyumbani zinafanywa na wanawake na zinayagusa mazingira moja kwa moja.
Nimezungumza na baadhi ya wakina mama ambapo wanasema mwanamke ni mlizi na mtu anaetakiwa kuyajali mazingira si kwa kupanda miti tu katika mazingira ya nyumbani bali hata kuotesha mbogamboga napo kuna mfaa zaidi.
Kila machi 8 Dunia huadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu kabla ya kilele cha siku ya wanawake Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilieleza nafasi ya mwanamke katika kuhifadhi na kutunza Mazingira.