Adha ya maji yendelea kuwa kero kwa baadhi ya Vitongoji Chiwona
20 March 2024, 6:18 pm
Hayo yamefahamika baada ya Taswira ya habari kushuhudia adha hiyo ambayo imechangia wananchi kuendelea kutumia maji yasio safi na salama.
Na Seleman Kodima.
Adha ya kukosekana kwa maji safi na salama kwa baadhi ya Vitongoji vya kijiji cha Chiwona imesababisha wananchi wa maeneo hayo kutumia maji yasio safi na salama.
Vicent Chilewa ni Mwenyekiti wa chiwona anasema kuwa licha ya uwepo wa kisima kirefu cha maji bado kimeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi wa kijiji hicho.
Aidha amesema moja ya changamoto inayosababisha kisima hicho kushindwa kuhudumia kijiji kizima ni kutokana na mfumo wa nishati jua kuwa kikwazo .
Chilewa amesema kuwa vitongoji viwili vinalazimika kutumia maji ya visima vya asili .
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Mabwe wametoa wito kwa mamlaka ya maji kushughulikia adha hiyo kwani wanaweza kuathirika na magonjwa ya mlipuko.
Naye Diwani wa Kata ya Makang’wa Bw.Solomoni Machilika amesema kuwa tayari wamefanya jitihada ya kuomba kuchimbiwa kisima kingine cha Maji.