Ummy: Asilimia 9.8 ya watu nchini hawana vyoo
5 March 2024, 5:00 pm
Waziri Ummy amezielekeza mamlaka kuhakikisha zinasimamia vyema matumizi ya vyoo kwa wasafiri wawapo safarini kwa kuhakikisha mabasi yanasimama kwenye maeneo rasmi ikiwemo stendi za mabasi .
Na Mariam Kasawa.
Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 9.8 ya watu nchini hawana vyoo kabisa ambapo hali ni mbaya zaidi maeneo ya vijijini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu anasema asilimia 13.4 ya wakazi wa vijijini hawana vyoo kabisa ,tafsiri ya kiashiria hiki ni kwamba watu hawa ndiyo wanaojisaidia ovyo vichakani na maeneo mengine yasiyo rasmi.
Kauli ya Waziri wa Afya inanifanya kutembelea pembezoni mwa jiji la Dodoma ili kufahamu uelewa wa wananchi juu ya matumizi na ujenzi wa vyoo bora.
Nafika katika Mtaa wa Muungano uliopo kata ya Mnadani nakutana na baadhi ya wananchi ambao wanadai kuwa hali duni ya maisha inachangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushindwa kujenga vyoo bora.
Kampeni ya nyumba ni choo imesaidi katika baadhi ya maeneo wananchi kuelewa matumizi ya vyoo bora viongozi wa maeneo wanasemaje kuhusu matumizi ya vyoo bora kwa wananchi.
Waziri Ummy amezielekeza mamlaka kuhakikisha zinasimamia vyema matumizi ya vyoo kwa wasafiri wawapo safarini kwa kuhakikisha mabasi yanasimama kwenye maeneo rasmi ikiwemo stendi za mabasi na vituo maalum pamoja na kupiga marufuku tabia ya wasafiri kujisaidia hovyo maarufu kama kuchimba dawa kwani ni aibu kwa Taifa na pia udhalilishaji wa utu.