Maji safi mwarobaini wa kupambana na magonjwa ya mlipuko
16 February 2024, 4:33 pm
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani katika ripoti yake ya mwaka 2015 Asilimia (81%) ya watu wanaokunywa maji ambayo si salama na huishi katika maeneo ya vijijini pamoja na kwenye makazi holela.
Na Mindi Joseph.
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama imebainika kuwa mwarobaini katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu kwa lengo la kulinda afya ya jamii.
Dodoma Tv imezungumza na wananchi wilayani kongwa na wamesema kipindi cha nyuma walikuwa wanachota maji kutoka vyanzo mbalimbali visivyo kuwa salama ikiwemo maji ya madimbwi hali iliyopelekea kuwa na changamoto ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara na kutapika.
Bashiri Salum ni Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma amesema katika kuhakikisha maji yanakuwa safi na salama kwa afya ya binadamu huwa yanawekewa dawa ya Klorini ambapo yamekuwa yakitumika kwa matumizi mbalimbali .