Saratani ya mlango wa kizazi tishio kwa wanawake
5 February 2024, 6:27 pm
Kila Februari 4 huwa ni maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambapo serikali imetoa rai kwa jamii kuchukua hatua za mapema kupima ugonjwa wa saratani, ambapo saratani ya mlango wa kizazi ni moja kati saratani zinazowapata akina mama.
Na Yussuph Hassan.
Imeelezwa kuwa katika kila Wagonjwa 100 wenye Saratani 25 ni Wanawake wenye Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambapo taarifa hiyo pia imebainisha kuwa Saratani ya Mlango wa kizazi inaweza kuwapata Wanawake na Wasichana ambao tayari wameanza kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi.
Taswira ya habari imefanya mahojiano na Wakazi Mkoani Dodoma kufahamu uelewa wao juu ya viashiria vya Saratani hii.
Neema Msemo Afisa Muuguzi kituo cha Afya Makole anafafanua juu kwa undani juu Saratani.