Senyamule akabidhiwa miradi ya BOOST wilayani Bahi
5 July 2023, 3:31 pm
Senyamule amepongeza uongozi wa wilaya ya Bahi kwa mshikamano ambao umewafanya kuwa wa kwanza kukamilisha miradi hiyo.
Na Bernad Magawa
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amekabidhiwa jumla ya madarasa 51, vyoo 63, majengo 2 ya utawala pamoja na nyumba ya mwalimu moja yenye uwezo wa kukaa familia mbili wilayani Bahi vyote vikiwa na gharama ya shilini Billion 1.5 fedha kutoka serikali kuu (BOOST) baada ya miradi hiyo kukamilika.
Akizunungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi shule mpya ya msingi Bahi Misheni ikiwakilisha miradi yote ya BOOST wilayani humo Senyamule amepongeza uongozi wa wilaya ya Bahi kwa mshikamano ambao umewafanya kuwa wa kwanza kukamilisha miradi hiyo kwenye Mkoa wa Dodoma huku katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Ally Gugu naye akitoa pongezi.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gongwe akimkaribisha Mheshimiwa Senyamule katika mradi huo ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan huku Mbunge wa jimbo la Bahi Kenneth Nollo na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Donald Mejitii (MNEC) na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima nao wakaeleza mambo mbalimbali.
Awali Afisa elimu ya awali na msingi wilaya ya Bahi Boniface Wilson alieleza namna madarasa hayo yatakavyo punguza msongamano wa wanafunzi madarasani huku Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndonuu pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Bahi sokoni Sifaeli Mbeti wakizungumza kwa niaba ya wananchi.