Watumishi wa Afya waaswa kuepuka uchepushaji wa dawa zenye asili ya kulevya
11 May 2023, 5:06 pm
Mafunzo ya wasimamizi wa dawa tiba zenye asili ya kulevya yamehusisha wataalamu wa afya kutoka vituo mbalimbali Dodoma lengo ikiwa kuhakikisha dawa hizo zinaendelea kutumika katika lengo lako sahihi la kutibu.
Na Yussuph Hassan.
Wito umetolewa kwa watumishi wa afya kuepuka vishawishi vitakavyosababisha uchepushwaji wa dawa zenye asili ya kulevya ili kuokoa nchi dhidi ya wimbi la kutibu waraibu wa dawa za hizo.
Wito huo umetolewa na Nelson Bukuru Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya rufaa ya Dodoma General katika ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi wa dawa tiba zenye asili ya kulevya yaliofanyika Jijini Dodoma.
Dkt Nelson amesema kuwa dawa zenye lengo la kutibu zinapotumika tofauti zina athari kubwa kwa jamii.
Kwa upande wake Benedict Brash Kaimu Meneja TMDA kanda ya kati amesema mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wataalamu wa afya.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walikuwa na haya ya kusema.