Dodoma FM

Wanawake watakiwa kupambana na mmomonyoko wa maadili

14 April 2023, 11:51 am

Mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya wananawake Tanzania Mchungaji Asuta  Mshama. Picha na Fred Cheti.

Hivi karibuni serikali kupitia waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Mh Nape Nnauye ilisema kuwa Ushoga,Usagaji pamoja na mapenzi ya jinsia moja hayana nafasi nchini.

Na Fred Cheti.

Wito umetolewa kwa wanawake nchini kusimama katika nafasi zao katika ulezi wa familia ili kupambana na vita vya mmomonyoko wa maadili ikiwemo kukataa suala la mapenzi ya jinsia moja.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya wananawake Tanzania Mchungaji Asuta  Mshama wakati akizungumza na Dodoma Tv ikiwa ni sehemu maandalizi ya kongamano la maombi kwa ajili ya kuombea maadili mema kwa taifa

Sauti ya Mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya wananawake Tanzania

Aidha Mchungaji Mshama amewataka viongozi wa dini pia kusimama vyema katika nafasi zao kwa kukemea kwa nguvu zote suala la mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mh Nape Nnauye. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Mtafiti na mwanaharakati wa kupinga mmomonyoko wa maadili katika shirika hilo  bwana Vakama Daniel anaelezea ni kwa kiasi gani hali ilivyo kwa kupitia utafiti alioufanya katika suala la mmomonyoko wa maadili ikiwa ni pamoja na wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Sauti ya Mtafiti na mwanaharakati wa kupinga mmomonyoko wa maadili

.