Hatimaye mgogoro wa ardhi Kingale watatuliwa
21 March 2023, 4:50 pm
Baada ya mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kutatuliwa hatimaye zoezi la upimaji limeanza rasmi katika eneo hilo.
Na Nizar Mafita.
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kata ya kingale na jeshi la magereza wilayani humo, tayari zoezi la uwekaji alama za mipaka limeanza kufanyika.
Akizungumza katika hafla ya dua maalumu iliyoongozwa na Shekhe wa Wilaya ya kondoa Shekhe Mchalu kwa ajili ya kushukuru kumalizika kwa mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kingale na gereza la kinganga mbunge was Jimbo la Kondoa Khamis Makoa amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uwekaji wa mipaka ya kudumu
katika hatua nyingne Mbunge huyo amesema uwepo wa jeshi la magereza katika Kata ya Kingale ni fursa kwa wakazi wa Kata ya hiyo katika Kuchochea maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji kondoa MOHAMED KIBERENGE amewasihi wakazi wa kata hiyo kudumisha ushirikiano baina yao na jeshi la magereza ili kuepusha migororo isiyotakiwa.
Katika dua hiyo Shekh wa Wilaya ya Kondoa SHEKH Khamisi Mchalu amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuupokea mwezi mtukufu wa ramadhani na kwa kutenda yale yanayompendeza mwenyezi mungu.
Nao baadhi ya wananchi wakizungumza katika mkutano huo wameishukuru Serikali Kwa kuwasikiliza na kutatua mgogoro uliokuwepo baina yao na Jeshi la magereza.