Serikali kuboresha miundombinu ya mifugo katika ranchi ya Narco
15 March 2023, 6:21 pm
Uwekezaji huo wa serikali unalenga kufanya ufugaji wa kisasa zaidi wenye tija ambao utaleta manufaa kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Jumla ya Bilion 4.6 zimewekezwa katika ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Wilayani Kongwa ili kuboresha miundombinu ya Mifungo.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mifugo Dr Daniel Mushi anazungumzia uboreshaji huo wa miundombinu.
Kwa upande wake Meneja wa Ranchi hiyo ya Taifa Narco iliyopo wilayani Kongwa Bw. Elias Binamungu amesema wananchi wanaozunguka Ranchi hiyo ya Taifa wamenufaika zaidi na vitalu vya ufugaji.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema uwepo wa ranchi hiyo unasaidia kufanya ufugaji wa kisasa na kukabiliana na athari za kutofuga kisasa.
Ufugaji ni sehemu ya jadi ya wakazi wengi wa Wilaya ya Kongwa ambayo ni hazina kubwa kwao.