Dodoma FM

Bahi watakiwa kulima mazao yanayo stahimili ukame

19 December 2022, 8:35 am

Na; Benard Filbert.

Wakulima wa kata ya Bahi wilaya ya Bahi mkoani  Dodoma wameshauriwa kupanda mazao ambayo yanahitaji mvua kidogo ili kukabiliana na  mabadiliko ya hali ya hewa.

Ushauri huo umetolewa na Diwani wa Kata hiyo  Agustino Mdunuu wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mkakati wa kilimo katika kata hiyo.

Amesema wakulima wanatakiwa kufuatilia taarifa za mamlaka husika ikiwepo hali ya hewa ili kujua ni namna gani wanaweza kufanya kilimo cha mkakati

Hata hivyo amesema Mheshimiwa Rais ameagiza mkoa wa Dodoma kutoa kipaumbele katika zao la alizeti hivyo kila mkulima anatakiwa kufuata maelekezo.

.

Hivi karibuni Mkuu wa idara ya kilimo na mifugo na uvuvi wilaya ya Kongwa Bw Jackson Shija alinukuliwa akiwataka wakulima kufanya kilimo himilivu ambacho kinaendana na hali ya hewa ili kuepusha changamoto ya kukauka kwa mazao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

.

Wakulima nchini wanasisitizwa kufuatilia taarifa mbalimbali za mamlaka husika ikiwepo hali ya hewa ili kufanya kilimo cha mkakati.