Mila na desturi kandamizi bado ni hatari kwa jamii
1 December 2022, 7:49 am
Na; Lucy Lister.
Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wananchi jijini Dodoma wameeleza kuwa,bado kuna mila na desturi zinazokandamiza ustawi wa mtoto wa kike na mwanamke ikiwemo ukeketaji,kurithi wajane na kutopewa haki ya kurithi mali.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi hao ambapo wamesema ukeketaji na kurithi wajane ni moja ya tamaduni zinazoendelezwa na baadhi ya jamii suala ambalo linasababisha kuharibu ustawi wa kundi hilo.
.
Kwa upande wake Easter Samuel Majani ambae ni Mwenyekiti wa jukwaa la Wanawake(MJT) amesema Serikali imetoa utaratibu mzuri wa kutoa elimu kutoka kwenye mashirika na taasisi mbalimbali kwa ajili ya akina mama na wanawake wote wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.
.
Ameongeza kuwa kwa wanawake waliopo Vijijini elimu inawafikia kutoka kwenye mikutano mbalimbali inayofanyika kila mwaka na kuwahamasisha kufahamu namna ya kupingana na mila na desturi zinazowakandamiza.
.
Sambamba na hayo amesema kuwa zipo sheria zinazomkinga mwanamke anaefanyiwa vitendo vya ukatili.