Dodoma FM

Kanisa la FPCT lajenga kituo cha upimaji wa watoto wenye ulemavu

21 April 2022, 3:57 pm

Na; Mariam Matundu.

Kanisa la FPCT jimbo la Dodoma  kupitia mradi wake wa elimu jumuishi limefanikiwa kujenga kituo cha upimaji kwa watoto wenye ulemavu ikiwemo kwa watoto viziwi .

Jane Mgidange ni mratibu wa mradi huo amesema hatua hizo zilifikiwa katika awamu ya kwanza ya mradi kwa jiji la Dodoma ambapo kwa awamu ya pili wamelenga kuhakikisha watoto na wazazi wawe na uwezo wa kufanya utetezi wa kuomba kuwepo kwa mazingira rafiki katika elimu jumuishi.

.

Nae katibu wa kanisa la FPCT jimbo la Dodoma mchungaji Daud Msaha amesema kuwa ili kufanikisha malengo ya mradi huo ni muhimu kuwepo na ushirikiano na wadau wote wa elimu hususani elimu jumuishi.

.

Kwa upande wake afisa elimu maalumu jiji la Dodoma Issa Kambi amesema  analipongeza kanisa hilo kwa kuja na mradi huo huku akisistiza kuweka nguvu pia katika kutoa mafunzo ya namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye changamoto za kujifunza kwani kundi hilo linapitia ukatili mkubwa .

.

Awamu ya pili ya mradi huu itatekelezwa kwa miaka minne 2022 hadi 2025 katika wilaya ya Bahi na Dodoma ukijikita zaidi  katika shule za msingi.