Jamii yatakiwa kuwafundisha watoto mambo mbalimbali ya kijamii wakati wa likizo
13 December 2021, 3:03 pm
Na; Benard Filbert.
Jamii imeshauriwa kuunga mkono kauli ya Serikali kuto kuwapeleka Watoto kusoma masomo ya ziada kipindi cha likizo na badala yake watumie muda huo kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.
Ushauri huo umetolewa na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma Dokta Allon Urio wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu suala la Serikali kuzia watoto kusoma masomo ya ziada kipindi cha likizo.
Dokta Urio amesema nia ya Serikali kutoa tamko hilo ni kutaka wanafunzi watumie muda wa likizo kujifunza vitu vingine vya kijamii lakini baadhi ya watu wamepokea kwa mtazamo tofauti kitu ambacho sio sawa.
Amesema kuna muda mwanafunzi anatakiwa ajifunze vitu tofauti na masomo kwani vitamsaidia katika maisha yake baada ya kuhitimu masomo yake.
Baadhi ya wazazi wakizungumza na taswira ya habari wamesema ni sawa watoto wanahitaji kujifunza vitu vya kijamii hususani kipindi cha likizo na sio wakati wote kuwa bize na masomo.
November 26 waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu aliwaagiza wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote Nchini kuhakikisha wanasimamia suala la wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya kijamii.