Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuacha imani potofu juu ya mtoto anae zaliwa na tatizo la mdomo wazi.

10 December 2021, 12:50 pm

Na ;Benard Filbert.


Wakazi jijini Dodoma wameiomba serikali kutoa elimu ya kutosha katika jamii kutokana na imani potofu hususani kwa watoto wenye tatizo la mdomo wazi ambao wamekuwa wakihusishwa na imani za kishirikina.

Hayo yameelezwa na wakazi hao wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu mapokeo hasi ya juu ya tatizo la mdomo wazi katika jamii.
Wamesema familia nyingi zikikumbwa na tatizo la mdomo wazi wamekuwa na imani potofu huku baadhi wakilalamikia kurogwa.

Hivi karibuni taswira ya habari ilizungumza na dakatari bingwa wa upasuaji midomo wazi kutoka hospital ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma Athanase Masele alisema jamii iache mtazamo huo badala yake inapogundua tatizo hilo wawapeleke wahusika hospital ili kupatiwa ufumbuzi.

Jamii inaombwa kuacha imani potofu kuwa mtoto akizaliwa na tatizo la mdomo wazi na kuamini kuwa amerogwa jambo ambalo sio kweli
Na ;Benard Filbert.