Kuchangia dawa ya meno kwa watu wengi ni njia mojawapo inayoweza kuchangia maambukizi ya uviko 19
18 October 2021, 12:11 pm
Na; Selemani Kodima.
Inaelezwa kuwa utumiaji na kuchangia dawa ya meno kwa watu wengi ni njia mojawapo inayoweza kuchangia maambukizi ya ugonjwa uviko-19 .
Hayo yamesemwa na Dkt Baraka Nzobo mtaalamu wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa kutoka wizara ya Afya ambapo amesema iwapo kuna mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa uviko-19 pasipo yeye kufahamu kuna uwezekano mkubwa kuweza kueneza ugonjwa huo kupitia uchangiaji wa dawa ya meno .
Aidha amesema kuwa kitendo cha mtu mmoja kushika tyubu ya dawa za meno mara kwa mara inasababisha kutapaka kwa virusi vya corona na kufanya Virusi hao kukaa nje ya tyubu .
Dkt Nzobo amesema ni vyema jamii kufikiria njia tofauti ya kuacha kuchangia tyubu ya mmoja ya dawa za meno hususani katika maeneo shuleni,kwenye kambi za wazee,vyuoni
Kwa upande mwingine amewataka wananchi kuwa makini na kuzingatia usafi katika utumiaji wa vyoo vya kisasa kutokana na virusi hivyo kuishi kwenye kinyesi ,
Pamoja na hayo Dkt Nzobo amesema tangu ugonjwa huo umeingia hapa nchini ,yapo mambo mengi yamebadilika hivyo ipo haja jamii kuchukua tahadhari na kuamua kuchanja chanjo ili kupunguza uwezakano wa kupata Virusi vya Uviko-19.