Jamii yatakiwa kuzingatia Afya ya Macho
15 October 2021, 11:59 am
Na; Shani Nicolous.
Wito umetolewa kwa jamii kuzingatia afya ya macho kwa kupima mara kwa mara macho .
Akizungumza na Taswita ya habari meneja wa mpango wa taifa wa huduma ya macho wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr. Benadertha Shillo amesema kuwa watu watengeneze desturi ya kupima afya ya macho mara kwa mara.
Amesema kuwa watoa huduma katika vituo mbalimbali vya afya wahakikishe huduma bora zinapatikana na kuhakikisha watu wenye ulemavu au shida yoyote wafike kituoni kwa urahisi.
Amesema watu wanachukulia kawaida kupata shida ya macho hasa makengeza kwa kuona kama ni shida ya kuzaliwa nayo bali tatizo hilo linatibika na lisipotibika hasa kwa watoto litaleta madhara makubwa baadaye hasa ya kukosa fursa ya kutimiza ndoto ya kuendesha ndege.
Kwa upande wake mtaalamu wa macho kutoka hospitali ya rufaa Dodoma Dr. Denis Nachipyangu amesema kuwa watu wazingatie neno ZUKITUKI lililobebea ujumbe mzito wa zuia ,kinga ,tunza macho kwani litawafanya kukumbuka kupima macho mara kwa mara na kupata tiba.
Madhimisho ya siku ya afya ya macho duniani hufanyika kila alhamisi ya pili ya mwezi wa kumi ambapo kidunia ili fanyika jana na kitaifa bado inaendelea yenye lengo la kuhakikisha uwepo wa huduma za macho zinazofikika kwa kila mwenye tatizo ,na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “PENDA MACHO YAKO KILA MMOJA ANAHUSIKA NENDA KAPIME SASA”