Zaidi ya Asasi 1000 zinatarajia kushiriki katika wiki ya Azaki 2021 jijini Dodoma
12 August 2021, 11:15 am
Na;Mindi Joseph .
Zaidi ya Asasi 1000 zinatarajia kushiriki katika wiki ya azaki mwaka 2021 Jijini Dodoma ili kuleta uelewa wa mchango wa asasi za kiraia Nchini.
Akizungumza mapema leo na waandishi wa habari Jijini Dodoma kwa niaba ya kamati ya maandalizi Bi. Recho Changonja Mkurungezi mtendaji wa haki Rasilimali amesema wiki ya azaki mwaka huu imekuja na nguvu mpya baada ya mwaka jana kutofanyika kutokana na ugonjwa wa Uviko 19.
Kwa upande wake Nesia Mahenge Mkurungezi Mkazi CBM Tanzania amebainisha kuwa katika wiki ya Azaki watatoa tuzo kwa mashirika mbalimbali Nchini ambayo yametoa mchango mkubwa kwa wananchi kusaidia maendeleo pamoja na vyombo vya habari.
Naye Mwakilishi wa Msajili wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii Faki Shaweji amesema wanaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa asasi zote Nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni.
Akizungumzia tahadhari zitakazozingatiwa na asasi zote katika wiki ya azaki na washiriki katika kujilinda na ugonjwa wa uviko 19 Nuria Mshare Mjumbe wa kamati ya maandalizi amesema watahakikisha wananchi na washiriki wanajikinga na ugonjwa wa uviko 19.
Wiki ya azaki Nchini inatarajiwa kufanyika octoba 23 hadi 29 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma huku zaidi ya wananchi 3000 wakitarajiwa kushiriki.