Dodoma FM

TCRA yatoa somo kwa waandishi wa habari masuala ya uchaguzi

7 November 2024, 5:54 pm

Na Anwary Shabani.                                             

Mamalaka ya Mawasiliani Tanzania TCRA  imewataka waandishi wa habari kuzingatia kanuni za utangazaji katika kuripoti na kutangaza masuala ya chaguzi zijazo.

Meneja wa huduma za utangazaji TCRA Mhandisi Andrew Kisaka amesema hayo katika mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika katika chumba cha habari Dodoma  Media Group jijini Dodoma.

Meneja wa huduma za utangazaji TCRA Mhandisi Andrew Kisaka katika mafunzo ya waandishi wa habari juu ya masuala ya uchaguzi
Sauti ya Mhandisi Andrew Kisaka

Baada ya kupatiwa mafunzo hayo , baadhi waandishi wa habari kutoka Dodoma Media Group  walieza jinsi umuhimu wa mafunzo hayo.

Pichani Bi. Mariam Matundu Mtangazaji wa Dodoma TV akielezea umuhimu wa mafunzo ya habari za uchaguzi
Suti za watangazaji
Pichani mtangazaji wa Dodoma TV Bernad Filber akielezea mambo muhimu ambayo amejifunza juu ya masuala ya uchaguzi.

Aidha Meneja wa Dodoma Media Group Bi. Zania Miraji amepongeza TCRA kwa kutoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya utoaji wa taarifa za uchaguzi.

Pichani Meneja wa Dodoma Media Group Bi. Zania Miraji akishukuru TCRA kwa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya uchaguzi
Sauti ya Bi Zania Miraji

Pamoja na hayo waandishi wa habari wamekumbushwa kuendelea kusoma na kujifunza mambo mapya kila siku ili kukuwa katika tasnia ya habari.