Serikali yajizatiti kutatua changamoto za vijana balehe
1 November 2024, 6:51 pm
Na Mariam Kasawa.
Serikali imejidhatiti kutatua changamoto zinazowakumba vijana balehe kwa kuweka mazingira salama na rafiki kwa vijana kupitia afua mbalimbali zinazowawezesha vijana kufikia malengo yao na utimilifu wao kwa ujumla.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amebainisha hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wanaotekeleza Afua za Vijana Balehe nchini (NAIA)kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Wakili Amon Mpanju, amesema miongoni mwa nguzo kubwa ambayo inapewa kipaumbele ni pamoja na kuzuia aina zote za ukatili wa aina ya kimwili pamoja na kuzuia vitendo vyote vya ukatili.
Kaulimbiu ya mkutano huo inayosema ”Utatuzi wa Changamoto za Vijana balehe kwa taifa imara” inachechemua utekelezaji wa Ajenda hii kwa upana wake kwa kuwa ndiyo pekee yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo za vijana kwa sasa . Mkutano huo unafanyika kuanzia 31 Oktoba hadi 01 Novemba ,2024 Mkoani Dodoma.