Dodoma FM

PM Majaliwa awataka vijana  kuchangamkia fursa za teknolojia

14 October 2024, 7:57 pm

Na Mindi Joseph.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana wachangamkie fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia katika kujipatia kipato na kushiriki kukuza Uchumi wa Taifa .

Amesema hayo Octoba 11 wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa uliyofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihurubia katika Wiki ya Vijana Kitaifa viwanja vya furahisha jijini Mwanza
Sauti ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amewataka vijana watumie  vizuri mifumo ya kidijitali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete
Sauti ya Mhe.Ridhiwani Kikwete