Wakazi wilayani Chamwino wanatarajia kunufaika na mradi wa boresha lishe
26 April 2021, 5:52 am
Na; Selemani Kodima.
Wakazi wa kijiji cha Chanhumba wilayani Chamwino wamesema wanatarajia kupata Elimu zaidi juu ya Lishe bora kupitia mfululizo wa Vipindi vya Redio vya Dodoma fm ili kusaidia kupunguza hali ya udamavu katika maeneo yao .
Wakizungumza na Dodoma fm baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wameweka wazi matarajio yao baada ya kuanza rasmi kwa kipindi cha Boresha lishe ambacho kinarushwa na Dodoma fm redio ambapo wamesema kupitia kipindi hicho wanatarajia kuelimika zaidi .
Keneth Chimbe na Monika Ghabula ni wakazi wa Chanhumba wao wamesema elimu ya Lishe bora ni mkombozi wa kupunguza hali ya udumavu kwa watoto chini ya Umri wa miaka mitano hivyo kupitia Kipindi cha BORESHA MAISHA itakuwa sehemu ya Darasa tosha kwao
Kwa upande wake afisa lishe wa wilaya ya Chamwino Bi Benadertha Petro ambapo mfululizo wa vipindi vya Boresha lishe vinafanyika katika eneo lake amesema lengo la vipindi hivyo ni kulega jamii yote ya chamwino katika kata 18 ,kwenye vijiji 39 huku walengwa wakuu wakiwa ni akina mama wajawazito, akina Mama wanaonyonyesha na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
amesema Hayo yanajiri baada ya kufanyika tafiti wa mwaka 2010 katika eneo hilo na kuonesha kuwa kuna tatizo la utapiamlo hasa udamavu .
Wiki hii Dodoma fm redio imeanza Rasmi kurusha Vipindi vinavyotoa Elimu ya lishe bora ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa Vipindi vya redio ambavyo vinawezeshwa na Mradi wa boresha lishe kwa ufadhili wa shirika la chakula duniani WFP ,TAHEA,RECODA ,FARM RADIO INTERNATIONAL NA SERIKALI YA MKOA WA DODOMA.