Dodoma FM

Serikali yahimiza klabu za maadili shuleni

19 September 2024, 7:52 pm

Kuwalea watoto katika malezi mema imetajwa kujenga kizazi bora na chenye maadili ambacho kitafuata mila na desturi la taifa letu.

Na Mindi Joseph

Moja ya jukumu la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kukuza maadili kwa watoto jukumu ambalo limetiliwa mkazo na Serikali ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na kizazi chenye kuishi kwa kufuata misingi ya maadili.

Afisa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Christiani Kaper  
Sauti ya Bwn.Christiani Kaper  

Modesta Mtui Afisa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma anabainisha kuwa jamii inaweza kumwandaa mtoto kuwa kiongozi bora wa baadaye.

Bi. Modesta Mtui Afisa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
Bi. Modesta Mtui Afisa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi

Mmomonyoko wa Maadili kwa watoto unasababishwa na nini?  je ni malezi Desderia Haule amabaye pia ni Mzazi na Afisa maadili anabainisha mambo yanayochangia mmomonyoko wa maadili kwa mtoto.

Bi. Desderia Haule Afisa maadili
Sauti ya Bi. Desderia Haule Afisa maadili

Malezi bora ya mtoto yanatokana na mzazi/mlezi anapomfundisha mtoto yale yote yaliyo mema ambayo yatamjenga katika maadili na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.