Dodoma FM

Shekimweri alaani tukio la mauaji Nala

17 September 2024, 8:59 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabiri Shekimweri

Uchunguzi ambao unaendelea kufanywa na jeshi la Zima Moto na Uokoaji ukishirikiama na vyombo vingine unaonesha kuwepo kwa viashiria vya kulipiziana visasi.

Na Nazael Mkude.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabiri Shekimweri amelaani tukio la mauaji lililotokea 16 Septemba 2024, Kata ya Nala alipotembelea eneo la tukio na kuzungumza na wananchi.   

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Mh. Shekimweri

.Diwani wa Kata ya Nala Helman Masira amekiri kumekuwepo na matukio ya mauaji ya mara kwa mara katika Kata hiyo wakati akibainisha mikakati mbalimbali ya kiulinzi waliyojiwekea ili kudhibiti hali hiyo.

Diwani wa Kata ya Nala Helman Masira
Sauti ya Diwani wa Kata ya Nala Helman Masira

Afisa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Inspecta Deogratius Peter Inanu amesema uchunguzi ambao unaendelea kufanywa na jeshi hilo unaonesha kuwepo kwa viashiria vya kulipiziana visasi.

Sauti ya Inspecta Deogratius Peter Inanu

Wanaotajwa kufariki katika tukio hilo la mauaji ni pamoja na Fatuma Mohamed (23), Dada wa kazi aliyefahamika kwa jina moja la Mkiwa, (18), Mtoto wa mwenye nyumba aliefahamika kwa jina la Milika Robert (12) na majeruhiwa ambao ni Rusajo Mwasongwe ambaye ni mama wa familia pamoja na mtoto wake ambae alitambulika kwa jina la Robart (6)

Picha kuonesha eneo la tukio la mauaji