Dira ya maendeleo ya 2050 izingatie usawa katika kila sekta
28 August 2024, 8:36 pm
Dira ya maendeleo mwaka 2050 inapaswa kuboreshwa katika mabo mbalimbali ikiwemo elimu na Afya.
Na Mariam Kasawa.
Wadau wameeleza maoni yao katika Dira ya mwaka 2050 kuwa inapaswa kuzingatia usawa kwa watu wote bila upendeleo kwa watu walio chini na wajuu wote wapatiwe huduma sawa.
Akiongea katika leo katika viwanja vya sabasaba katika Tamasha la 7 la jinsia ngazi ya wilaya Kaimu mkuu wa Idara ya ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Bi. Flora Ndaba amesema Dira ya maendeleo mwaka 2050 inapaswa kuboreshwa katika mabo mbalimbali ikiwemo elimu na Afya.
Aidha Bi Ndaba anasema bado kuna vizingiti vinavyo zuia wananchi kuzifikia fursa za kiuchumi hali inanyo pelekea fursa hizi kukumbatiwa na watu wachache na kushindwa kuwafikia wananchi.