Kipindupindu chatajwa kuwakumba wanawake zaidi nchini
29 January 2024, 8:00 pm
Kipindupindu unatajwa kuwa ugonjwa hatari ambao huambatana na kuharisha na kutapika huku ikielezwa kuwa ni asilimia 10 tu ya wagonjwa wanaopata kipindupindu na kulazwa hospitali huku wengine wakitembea na vimelea vya ugonjwa huo.
Na Mariam Matundu.
Wanawake nchini Tanzania wanatajwa kuongoza kwa asilimia 49.6 kupata maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu kutokana na shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Wakati ikielezwa kuwa kipindupindu huashiria hali ya umasikini huku ukubwa wa tatizo la mlipuko wa ugonjwa huo ukitajwa kuchukua takribani million 1.3 ya nchi duniani na Tanzania ikiwemo.
Bi. Theresia Masoi ni mtafiti kutoka chuo kikuu cha Dodoma hapa anaelezea maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huu huku akieleza zaidi ni kwanini wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa huu.
Umuhimu wa kupanga bajeti ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu nao unatajwa kuwa nuhimu zaidi hususani kwa serikali kama anavyoeleza Bw. France Lasway mchumi kutoka Wizara ya Afya .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Bi Rose Reuben akapata wasaa wa kuilezea kwa ufupi maana ya MEDIA SCIENCE CAFEE ambayo imekuwa ikiwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali .