Jiji la Dodoma laendeleza jitihada za kupambana na udumavu
15 January 2024, 8:28 pm
Tafiti hizi zinafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351 ambayo inaipa mamlaka ya Kisheria ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kufanya tafiti mbalimbali za Kitakwimu.
Na Alfred Bulahya.
Imeelezwa kuwa mkoa wa Dodoma bado unakabiliwa na tatizo la udumavu huku jitihada za kuhakikisha tatizo hilo linatokomezwa zikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akifanya Mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuzungumzia utafiti wa shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanyika katika mikoa yote ukiwemo Mkoa wa Dodoma.
Tafiti hizi zinafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351 ambayo inaipa mamlaka ya Kisheria ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kufanya tafiti mbalimbali za Kitakwimu ili kuzalisha Takwimu kwa ajili ya kutumika katika kutunga na kuhuisha sera, kupanga mipango na programu za maendeleo na kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake.