Dodoma FM

Wanafunzi kidato cha kwanza kupokelewa shuleni bila kujali mapungufu ya mahitaji yao

8 January 2024, 8:47 pm

Picha ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mwl. Easter Simchimba akiongea na Dodoma Tv. Picha na Fred Cheti.

Mzazi anaweza kumpeleka mtoto hata kama hajakamilisha mahitaji yote ili aweze kuanza masomo wakati taratibu za kukamilisha mahitaji hayo zikiendelea.

Na Fred Cheti.
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza bila ya kujali mapungufu ya mahitaji aliyonayo ili aweze kuanza masomo.

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza bila ya kujali mapungufu ya mahitaji aliyonayo ili aweze kuanza masomo.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa shule ya Sekondari Viwandani iliyopo jijini hapa Mwl. Easter Simchimba wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv kuhusu muhula mpya wa Masomo uliofunguliwa leo ambapo amesema mzazi anaweza kumpeleka mtoto hata kama hajakamilisha mahitaji yote ili aweze kuanza masomo wakati taratibu za kukamilisha mahitaji hayo zikiendelea.

Sauti ya Mwl. Easter Simchimba .
Picha ni Wanafunzi wa shule ya sekondari viwandani Jijini Dodoma . Picha na Fred Cheti.

Katika hatua nyingine Mwalimu Easter amezungumzia jinsi ambavyo wamejipanga kuupokea ya mtaala mpya wa masomo ambapo unaotarajia kuanza mwaka huu.

Sauti ya Mwl. Easter Simchimba .

Nao baadhi ya wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza pamoja na wengine wa vidato vingine wamezungumzia jinsi ambavyo wamejipanga kuanza muhula huu mpya wa Masomo.

Sauti za Wanafunzi.