Wakazi wa Azimio waombwa kuwa watulivu sakata la mgogoro wa ardhi
13 December 2023, 8:17 pm
Hivi karibuni Waziri wenye dhamana ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh.Jerry Silla alielekeza watendaji wa sekta ya ardhi nchini kuhakikisha ndani ya siku mia moja kuanzia Sept 4-2023 wanatatua migogoro ya ardhi kwa kadri ya uwezo wa nafasi zao.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa mtaa Azimio Kata ya Ipala wameombwa kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mkanganyiko wa mgogoro wa ardhi baina yao na Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mh.John Kayombo alipokuwa akizungumza na wananchi wa mtaa huo na kuwatoa hofu juu ya dhana walinayo ya kuonewa na Serikali
Kayombo amesema kuwa ingawa eneo hilo lilitengwa kama eneo hifadhi ya akiba lakini mamlaka husika inaweza kubadili matumizi ya ardhi kwa mujibu wa sheria hivyo haina haja ya wananchi kuona hilo likifanyika
Aidha amewaomba wananchi wa mtaa huo kudumisha amani ya nchi na kuachana na vitendo vya uvunjifu wa amani kwa watumishi wanaofika eneo hilo
Naye Diwani wa Kata ya Ipara Bw.George Magawa amewaomba wananchi wake kufuata taratibu za kudai haki na kuacha kuvunja sheria kwa kujichukuria sheria mkononi kwani hiyo itawagharimu