Wakazi wa Nholi waaswa kuepuka migogoro ya ardhi
18 October 2023, 9:48 am
Kupitia zoezi la urasimishaji wa ardhi nchini itasaidia kutoa hati ya umiliki wa vipande vya ardhi na kupunguza changamoto za kugombania na mashamba.
Na Victor Chigwada.
Wito umetolewa kwa wananchi wa kijiji cha Nholi kuepukana na migogoro ya ardhi kwani imekuwa ikipelekea kuvunjika kwa amani na hata kusababisha mapigano.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Bahi Mh.Keneth Nollo alipo kuwa akizungumza na wananchi wa Nholi licha ya kusema kuwa baadhi ya mogogoro inachagizwa na viongozi wa vitongoji na vijiji.
Aidha amesema migogoro mingine imekuwa ikitokana na ubabe wa baadhi ya wananchi na kijikuta wanaleta madhara makubwa kwa jamii.
Nollo ameongeza kuwa hakuna kiongozi wa ngazi ya kijiji,wilaya hata anayeweza kutoa hukumu ya mdomo juu ya mgogoro wa ardhi unao husisha pande mbili.
Amehitisha kwa kusema kuwa ni vyema kila mtu kulinda utu na kuacha kuanzisha migogoro ya ardhi kwani kusababisha maafa yanayo tokana na ardhi ni kujisababishia laana ya vizazi na vizazi.
Nao baadhi ya wananchi wakiwa katika utatuzi wa mgogoro wa ardhi wameiomba Serikali kuendelea na zoezi la urasimishaji ardhi nchini kote ili kuondokana na migiogoro isiyo ya lazima.