Rasimu mkakati wa kilimo ikolojia yatakiwa kuwa katika lugha rahisi
26 September 2023, 3:57 pm
Kongamano hilo limejumuisha wadau wa kilimo na wakulima kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania mkakati wa kilimo hai unatarajia kuja na majibu juu ya kilimo hai .
Na David Kavindi.
Imeelezwa kuwa rasimu ya mkakati wa kilimo ikolojia hai inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili iwe katika lugha rahisi itakayoeleweka kwa wakulima .
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo chini Bw. Obadiah Nyegiro ambapo ameyasema kuwa hayo katika uzinduzi wa kongamano la kilimo hai ikolojia ulilofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena hotel ambapo amewataka wadau wanaosimamia mkakati wa kilimo ikolojia hai kuzingatia lugha rahisi itakayoeleweka kwa wakulima kwa ajili ya utekelezaji.
Naye mwenyeketi wa kamati ya uandaaji wa kamati ya taifa ya kilimo ikolojia hai Bw. Levelen Ngaiza ameeleza malengo ya mkakati huo ni kuhakikisha kama Taifa linazalisha chakula na kuzingatia kulinda mazingira
Nao baadhi ya wadau na wakulima wa kilimo hai walioshiriki katika kongamano hilo wameiomba serikali kusimamia mkakati wa kilimo hai na kuongeza elimu juu ya makakati huo na kuongeza teknolojia iliku kusaidia wakulima wadogo kupata pemebejeo za kisasa