Wajawazito waonywa kuepuka matumizi ya Pombe
20 September 2023, 2:55 pm
Ili kupunguza vitendo vya matumizi ya pombe na dawa za kulevya katika jamii hususani kwa wajawazito wataalamu wa afya wanaendelea kuhamasisha jamii kuachana na suala hilo kwani lina athari kubwa kiafya.
Na Katende Kandolo.
Akina mama wajawazito wametakwa kuachana na matumizi ya pombe katika kipindi cha ujauzito kwani Inaweza kuwaletea athari za kiafya pamoja na kumdhulu mtoto aliyeko tumboni.
Nimekutana na Dokta Zahadi Shemahonge ambaye yeye ni daktari wa magonjwa ya akili kutoka katika Hospitali ya Mirembe kituo cha Itega.
Kwanza nilianza kwa kumuuliza je ni athari gani ambazo anaweza kupata mama mjamzito pale anapotumia vilevi na dawa za kulevya kipindi cha ujauzito?
Pamoja na mambo mengine hapa anatoa ushauri kwa akina mama,pamoja na wajawazito juu ya mambo ya kuepuka katika kipindi cha ujauzito.
Dodoma Tv imefanya mahojinao na baadhi wananchi jijini Dodoma juu ya mtazamo wao kuhusiana na suala la matumizi ya dawa za kulevya pamoja na pombe.