Jamii yatakiwa kuzingatia lishe bora
18 September 2023, 2:29 pm
Mara kadhaa Wizara ya Afya pamoja na taasisi mbalimbali za afya nchini zimekuwa zikitoa ushauri kwa jamii kuzingatia ulaji wa lishe bora lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kinga ya mwili.
Na Diana Massae.
Jamii imetakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora hususani kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani husaidia kuimarisha afya ya mwili na huongeza siku za kuishi.
Ushauri huo umetolewa na mtaalam wa lishe kutoka taasisi ya Agriculture Nutrition and Empowerment [ANUE] Bw. Mengo Chikombe Wakati akizungumza na Dodoma Tv ambapo amesema ni vyema kwa watu kuzingatia ulaji wa mbogamboga na matunda ili kuimarisha kinga ya mwili.
Katika hatua nyingine amesema wanaendelea kushirikiana na serikali ikiwemo Wizara ya Afya kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulaji wa lishe bora.
Dodoma Tv imekutana na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma ambapo wamesema hawana elimu juu ya kuzingatia ulaji wa lishe bora hivyo kutoa ushauri kwa waatalamu wa lishe Jijini Dodoma kutoa elimu kwa jamii juu ya suala hilo.