Wananchi wafunguka kufuatia kauli ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)
28 August 2023, 12:30 pm
Ikumbukwe kuwa, Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza mtu yeyote ambaye hatumikii Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala jeshi lolote lililowekwa kwa mujibu wa sheria kuvaa vazi rasmi la jeshi lolote katika hayo yaliyotajwa au vazi lolote linalofanana na vazi rasmi la majeshi hayo.
Na Abraham Mtagwa.
Wananchi Jijini Dodoma wamekuwa na maoni mbalimbali, kufuatia kauli ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyotolewa Agost 25 ya kutoa siku saba kwa Wananchi kusalimisha mavazi ya jeshi au yanayofanana na sare za Jeshi hilo.
Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya Wafanyabiashara wa Nguo kutoka soko la Machinga Complex wamesema kuwa suala la uuzaji wa nguo hizo limekuwa ni changamoto kubwa kuisha na hapa wanaeleza baadhi ya sababu zinazopelekea changamoto hiyo.
Aidha kituo hiki kimepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya Wananchi Jijini Dodoma ambao wametoa mitazamo mbalimbali kufuatia kauli ya Jeshi hilo huku wengi wakishauri udhibiti wa nguo au sare hizo uanzie sehemu mizigo inaposhushwa kutoka nje.
BW. Moses John, ambaye ni Mkazi wa Majengo jijini Dodoma ametoa ushauri kwa Watu wenye tabia ya kutumia Mavazi au sare za Majeshi mbalimbali Nchini kwa ajili ya kufanya uhalifu kuacha tabia hiyo kwani inahatarisha usalama wa maisha yao na maisha yaw engine.