Wamiliki wa mafuta waahidi kutoa ushirikiano wa kusambaza mafuta
25 July 2023, 4:30 pm
Wamiliki hao wameiomba serikali iimarishe upatikanaji wa dola ili zisaidie katika biashara hiyo.
Na Fred Cheti.
Wamiliki wa maghala ya mafuta nchini wameihakikishia Serikali kuhusu upatikanaji wa mafuta wakisema wana petroli na dizeli za kutosha na wapo tayari kutoa ushirikiano wa kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali yenye uhitaji.
Wamiliki hao wameyasema hayo mara baada ya serikali kupitia waziri wa Nishati Mhe. January Makamba kufanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhia mafuta ya Petroli na Dizeli
Wamiliki hao wamesema kuwa wanafanya kazi saa 24 hadi siku za mapumziko ili kuhakikisha magari yanaingia na kutoka katika maghala kwa lengo la kuchukua mafuta na kuyasafirisha katika maeneo mbalimbali huku wakiiomba serikali iimarishe upatikanaji wa dola ili zisaidie katika biashara hiyo.
Kwa upande wake waziri wa Nishati Mhe January Makamba amewapongeza wamiliki wa maghala hayo kwa kuendelea kutoa huduma hiyo huku akihaidi serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwao.