Mpango matumizi ya ardhi kupitia LTIP kiboko ya migogoro ya ardhi
24 July 2023, 1:10 pm
Mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi utawezesha haki kupatikana na kufanikisha uwepo wa ushirikiano wa familia kati ya mume na mke na upatikanaji wa hati za kimila .
Na Seleman Kodima.
Viongozi wa serikali za Mitaa wametakiwa kutoa ushauri thabiti na ushirikiano ili kufanikisha mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi (LTIP ) hatua itakayowezesha kutekelezwa kwa mradi huo
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mufindi, Frank Sichalwe ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ,wakati wa kikao cha wadau kujadili Rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambapo amesema kupitia kikao hicho maamuzi yatakayo tolewa yatatumika katika mpango wa matumizi ya ardhi katika maeneo yao
Aidha ametaja faida zitokanazo na mpango wa matumizi ya ardhi kwa halmashauri hiyo kuwa ni pamoja na kuondoa migogoro ya ardhi isiyokuwa na lazima hivyo amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuanzia madiwani kwena kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mpango huo.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wa mradi Kutoka Wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi ambayo amekuwa akisimamia masuala ya jamii kupitia mradi wa (LTIP) amesema maandalizi ya mpango wa matumiz ya ardhi unafaida kubwa katika jamii
Amesema mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi (LTIP ) umehusisha jamii mbalimbali katika maandalizi kupitia madodoso katika kuanisha maeneo mbalimbali katika wilaya zinazotekeleza mradi huo
Pamoja na hayo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi linafuata la uandaaji wa matumizi ya ardhi za vijiji kwa kuzingatia mpango wa matumizi ya ardhi wa wilaya .
Nae Diwani wa kata ya Igombavanu Veronica Kilungumtwa akizungumzia Mpango huo ambapo wamepata nafasi ya kushauri na kujadili kwa pamoja amesema kuwa mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi utawezesha haki kupatikana na kufanikisha uwepo wa ushirikiano wa familia katika mume na mke ,upatikanaji wa hati za kimila .