Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakandarasi wazawa
14 July 2023, 5:32 pm
Wakandarasi wazalendo nchini wameiomba serikali kuwapatia miradi mikubwa ili kutoa ajira kwa watanzania wengi.
Na Fred Cheti.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa serikali hasa ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakandarasi wazawa huku akiwataka wakandarasi hao kumaliza miradi wanayopewa kwa wakati
Mhe. Senyamule ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wakandarasi katika semina ya wakandarasi na wafanyabiashara iliyoandaliwa na moja ya benki nchini kwa lengo la kujadili namna ya kukuza uchumi kupitia miradi ya ujenzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wakandarasi wazalendo nchini Bwana Thobias Kyando ameiomba serikali kuwapatia miradi mikubwa ili kutoa ajira kwa watanzania wengi.