Mashirika yasiyo ya kiserikali yatakiwa kutumia fursa zinazojitokeza
26 June 2023, 5:09 pm
Asasi zaidi ya 50 mkoani Dodoma zimenufaika na mafunzo hayo ambayo yanalega kuongeza uelewa na namna ya kujua kujitafutia rasilimali.
Na Mindi Joseph.
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yametakiwa kutumia fursa zinazojitokea ili kuifikia jamii kwa ukaribu kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali halmashauri ya jiji la Dodoma Peter Pantaleomaria anasema mafunzo yanayotolewa kwa asasi za kiraia yanachangia kutekeleza kwa ufanisi miradi hiyo.
Baadhi ya wadau kutoka mashirika yasiyoyakiserikali wanasema mafunzo wanayoyapata ni nguzo kwao katika kuigusa jamii.
Mratibu wa mtandao wa asasi za kiraia mkoa wa Dodoma Edward Mbogo anasema mafunzo ni njia bora ya kuwezesha kufikia malengo waliyokusudia.