Dodoma FM

Mradi uchimbaji visima vya maji kunufaisha wakazi Nzuguni

1 June 2023, 5:38 pm

Zoezi la uchimbaji visima katika eneo la Nzuguni. Picha na Mindi Joseph.

Mradi huo wenye mikataba minne una thamani ya sh. Bilioni 4.8.

Na Mindi Joseph.

Wakazi 37,929 katika kata ya Nzuguni mkoani Dodoma wanatarajia kunufaika na utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa visima vya maji  unaotarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Katibu wa kata Chama cha Mapinduzi Nzunguni Fanuel Yoramu ameipongeza serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao utapunguza mgao na adha ya maji.

Amesema awali walikuwa wanakunywa maji ambayo yanatumiwa pia na mifugo.

Sauti ya Katibu wa kata Chama cha Mapinduzi Nzunguni.
Katibu wa kata Chama cha Mapinduzi Nzunguni Fanuel Yoramu . Picha na Mindi Joseph.

Gerald Mtemi ni mkazi wa Nzunguni anakiri kuwepo kwa shida ya maji na mradi huu utawasaidia.

Sauti ya mkazi wa Nzunguni .