Dodoma FM

Wakazi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanajilinda dhidi ya maambukizi ya Uviko 19

15 July 2021, 12:21 pm

Na;Yussuph Hans.

Rai imetolewa kwa wakazi wa Jijini la Dodoma kuhakikisha wanajilinda dhidi maambukizi ya virusi vya korona, kwa kuhakikisha wanapunguza safari zisizo na ulazima pamoja na kuvaa barakoa katika mikusanyiko.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri wakati akizungumza Dodoma Fm juu ya namna uongozi wa Jiji unavyoendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ugonjwa huo.

Shekimweri amesema ni vyema jamii ikajipangia utaratibu wa kununua bidhaa za kutosha na kuhifadhi ndani, ili kuepuka msongamano maeneno ya sokoni pamoja na wachuuzi na wauzaji kuhakikisha wanachukuwa tahadhari zote za kiafya.

Kwa upande wake afisa afya Jiji la Dodoma Bw. Abdallah Mahia amesema kuwa wamepanga kufikisha elimu kwa wakazi wote ndani ya Jiji la Dodoma kupitia njia mbalimbali ikiwepo kutumia vyombo vya habari.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wakazi Mkoani Dodoma na wamesema wamekuwa na muamko kwa sasa ambapo uvaaji wa barakoa katika mikusanyiko umeongozeka kama sehemu ya kujikinga na maambukizi hayo.

Tayari Serikali Imekwisha kuthibitisha kuwepo kwa maambukizi ya Virusi vya Corona katika baadhi ya Mikoa Nchini huku ikitoa wito kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zaidi