Dodoma FM

e- GA kuimarisha mtandao kwa miaka 10 ijayo

23 February 2023, 5:13 pm

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi. Benedict Ndomba. Picha na Habari Maelezo

Mamlaka ya Serikali Mtandao ina mpango wa kuhakikisha inajenga Serikali ya Kidijiti Katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imesema Katika kipindi cha miaka 10 ijayo itahakikisha huduma za mtandao maeneo yote zinapatikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi. Benedict Ndomba amesema wanaandaa na kutekeleza mikakati hiyo madhubuti ili kuimarisha zaidi utekelezaji huo.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi. Benedict Ndomba

Kwa upande wake Msemaji wa serikali Gerson Msigwa Naye amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao imesaidia kuondoa udanganyifu uliokuwa unafanyika katika ukusanyaji wa mapato.

Sauti ya Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Serikali Mtandao ni matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utendaji kazi wa Taasisi za Umma na utoaji wa huduma kwa wananchi