Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutumia fursa mwezi wa Ramadhani

11 April 2022, 4:11 pm

Na;Yussuph Hassan.

Wananchi Mkoani Dodoma wameshauriwa kutumia fursa zinazopatikana kupitia Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kupunguza ugumu wa maisha.

Ushauri huo umetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema katika msimu huu kuna fursa nyingi hivyo ni vyema wananchi wakachangamkia fursa hizo pasi na kuathiri uchumi wa watu wengine.

.

Aidha pia ameshauri jamii kuwasaidia watu wenye uhitaji katika kipindi hiki, kwani kuna faida lukuki za kufanya hivyo.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya Wakazi Mkoani hapa ambapo changamoto ya kupanda kwa bei za bidhaa imekuwa tatizo kwao huku wakiomba serikali kuangalia suala hilo kwa makini.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni moja ya ibada inayotekelezwa na waumini wa dini ya kiislamu duniani kote, ambapo kwa msimu imeonekana kuwa gharama za maisha zimepanda mara dufu kulinganisha na msimu uliyopita.