Dodoma FM

Serikali yatakiwa kushirikiana na mashirika binafsi ili kutokomeza vitendo vya ukatili

19 July 2021, 11:12 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa serikali kutengeneza umoja na mashirika binafsi pamoja na jamii nzima ili kutokomeza vitendo vya ukatili nchini.
Akizungumza na Dodoma fm meneja mradi wa shirika lisilo la kiserikli la {Action for community care} Bi, Stella Matemu amesema kuwa umoja na nguvu ya pamoja utasaidia kuweka nguvu ya kutosha katika kutokomeza ukatili katika jamii.
Amesema dini mbalimbali pia zinamchango mkubwa wa kukemea ukatili hivyo ni vyema viongozi wa dini wakatambua wajibu wao wakuleta mabadiliko katika hili.

Aidha amesema kuwa pamoja nakuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya kikatili lakini bado changamoto imekuwepo kwa watuhumiwa kuendelea kuwepo mtaani bila adhabu yoyote hali inayochangia wanajamii kukata tamaa ya kuripoti matukio ya ukatili.

Amewataka wanawake kuwa wepesi wa kuripoti pindi mtoto anapofanyiwa ukatili ili kukomesha vitendo hivi kwani ikibainika mama nae anafumbia macho suala hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Dodoma fm imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa ambao wamekiri kuwepo kwa vitendo hivi katika jamii hivyo ni vyema wazazi kuwa makini na watoto wao na kujua maisha halisi pamoja na njia zao zote wanazopita wakiwa nyumbani hata shuleni.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto vimebainika kukita mizizi katika wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma ambapo ripoti ya Wilaya hiyo inaonesha kuwa watoto 981 wamepewa ujauzito katika kipindi cha miezi sita iliyopita Januari mpaka Juni 2021.