Dodoma FM

Wakulima watakiwa kuwa na desturi ya kutoa taarifa kwa maafisa ugani, maendeleo ya mazao

29 April 2021, 6:52 am

Na; shani Nicolaus             

Wito umetolewa  kwa wakulima kuwa na desturi ya kutoa taarifa kwa maafisa ugani kuhusiana na maendeleo ya mazao pamoja na aina ya viuatilifu vya kutumia kuhifadhia mazao yao.

Akizungumza  na Dodoma fm Afisa kilimo mkoa wa Dodoma Bw. Bernad Abraham amesema kuwa ni vyema wakulima wakatoa ushirikiano kwa maafisa ugani ili kupewa ushauri wa namna ya kutunza na kuhifadhi mazao pamoja na changamoto nyingine zinazohusu kilimo.

Aidha ameongeza kuwa soko la zabibu halifanyi vizuri kutokana na tija ndogo kwenye uzalishaji hivyo wakulima wanatakiwa kutumia mbinu bora za kilimo  ili kuzalisha zaidi.

Kazi kubwa ya wataalamu wa kilimo katika ngazi mbalimbali ni kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima ambapo Serikali imepanga maafisa ugani katika ngazi ya Kijiji hadi Taifa ili kusaidia wakulima kulima kwa tija.