Dodoma FM

DC  Gondwe apiga marufuku wanafunzi kuchunga mifugo siku za masomo

16 March 2023, 3:39 pm

Mh. Godwin Gondwe mkuu wa wilaya ya Bahi akizungumza na wananchi wa Bahi Sokoni. Picha na Bernad Magawa.

ni vema wazazi kupunguza tabia ya kuwa wakali kwa watoto wao na badala yake wajenge  urafiki kwa kuzungumza nao mara kwa mara  ili  wasiwaogope , bali   wawe huru kwa wazazi wao  kueleza changamoto mbalimbali.

Na Benard Magawa

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mheshimiwa Godwin Gondwe amepiga marufuku watoto wote wenye umri wa kwenda shule  kuchunga  mifugo  siku za masomo na kuagiza wazazi kuhakikisha  watoto wao wanahudhuria shuleni kila siku   ili wapate elimu itakayowasaidia watakapokuwa watu wazima.

Mheshimiwa Gondwe ameyasema hayo mapema wiki iliyopita  alipokuwa akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Bahi sokoni kwa lenga  kusikiliza kero za wanachi.

Gondwe amewaomba wazazi, walezi, wiongozi wa dini, viongozi wa Serikali, na wazee wilayani humo kushirikiana katika kuhimiza na kusimamia  suala la elimu,  kwani serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya elimu hivyo ni vema watoto wote wa Tanzania wakanufaika na fursa ya elimu   bure bila kuikosa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe.

Aidha amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika maadili bora huku akisisitiza kuhakikisha wanapambana na suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto na akina mama ili kuwa na kizazi bora chenye maadili.

Mh. Godwin Gondwe mkuu wa wilaya ya Bahi akizungumza na wananchi wa Bahi Sokoni. Picha na Bernad Magawa.

Amesema ni vema wazazi kupunguza tabia ya kuwa wakali kwa watoto wao na badala yake wajenge  urafiki kwa kuzungumza nao mara kwa mara  ili  wasiwaogope , bali   wawe huru kwa wazazi wao  kueleza changamoto mbalimbali  wanazokutana nazo kuhusu ukatili wa kijinsia katika jamii.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe.

Amehimiza jamii ya wana Bahi  kupiga vita ukatili wa kijinsia kwani unawaharibu watoto wengi kisaikolojia na kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao katika masomo, amewasihi wananchi kuhakikisha  wanatoa taarifa kwa vyombo vya sheria kuhusu matukio yote ya ukatili wa kijinsia  ili yaweze kuchukuliwa hatua kwa za haraka.