Dodoma FM

Wamiliki wa kumbi za starehe watakiwa kuzingatia sheria

13 March 2023, 11:37 am

wamiliki wa biashara hizo, jijini Dodoma katika mkutano uliowakutanisha na baadhi ya watendaji wa kata wakiwemo maafisa afya na maafisa wa jeshi la polisi. Picha na Fred Cheti.

Hii inajiri kufuatia kuwepo kwa baadhi ya malalamiko ya wanachi ya jijini la dodoma kuhusu baadhi ya kumbi za starehe ambazo nyingi zipo katika makazi ya watu kupiga mziki kwa sauti ya juu na kusasbabisha kero kwa wanachi.

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imewataka wamiliki wa kumbi za starehe, migahawa pamoja na nyumba za wageni kuzingatia taratibu katika utoaji wa huduma hizo ili kuondoa usumbufu na kero kwa wananchi

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri wakati akizungumza na wamiliki wa biashara hizo jijini Dodoma katika mkutano uliowakutanisha na baadhi ya watendaji wa kata wakiwemo maafisa afya na maafisa wa jeshi la polisi.

Sauti yaMkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri

Aidha Mh Shekimweri ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki hao kushiriki katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti katika baadhi ya maeneo ya seheo zao za biashara

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri .

Kwa upande wake Afisa biashara wa jiji la Dodoma amechangua mida ambayo sehemu hizo za satarehe hasa zinazouza vileo zinapaswa kufunguliwa na kufungwa kwa ajili ya utoaji huduma

Sauti ya Afisa biashara wa jiji la Dodoma

Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dk Samweli Gwamaka wakati akieleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka miwili alibainisha kuwa NEMC imepokea malalamiko 369 ya wananchi kuhusu uchafuzi na uharibifu wa mazingira ikiwemo kelele za muziki kwenye nyumba za starehe huku akieleza kushamiri kwa gereji bubu katika maeneo ya makazi