Dodoma FM

Urasimishaji ardhi ni changamoto kwa wananchi wasio kuwa na elimu juu ya zoezi hilo

10 August 2022, 2:33 pm

Na; Victor Chigwada.

Pamoja na faida za urasimishaji na upimaji wa ardhi nchini lakini zoezi hili limekuwa na changamoto kadhaa wa kadha kwa baadhi ya maeneo kutokana na uelewa mdogo wa wananchi

Taswira ya habari imezungumza na Jane samsoni  ambaye amekiri licha ya zoezi la urasimishaji na upimaji viwanja kukamilika lakini kumekuwa na mkanganyiko kwa wananchi Hali inayosababisha  kuibua migogoro

.

Bi Samsoni ameiomba Serikali kupitia Halmashauri  kuingilia Kati zoezi Hilo kwani wananchi wengi wanalalamika kuonewa na kuchukuliwa viwanja vyao

.

Aidha mjumbe mwakilishi wa kitongoji Cha Ndwene Bw.Gidioni Nyagalu amekiri kukumbana na changamoto ya uelewa wananchi juu ya suala la upimaji viwanja hali inayochagia kukosekana kwa barabara za mitaa

.

Ameongeza kuwa pamoja na zoezi Hilo kupokelewa na wananchi  lakini mizozo imekuwa mingi kutokana na baadhi ya wananchi viwanja vyao kuhamishwa .

.