Dodoma FM

Wilaya ya Mpwapwa yapongezwa kwa kufanya vizuri katika anuani za makazi

11 July 2022, 1:46 pm

Na; Alfred Bulahya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Kata ya Pwaga na Luhundwa iliyolenga kutembelea na kufanya Mikutano na wananchi ili kusikiliza kero zao.

Amesema Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kutambua   ramani za mitaa, na barabara zilipo hivyoamewapongeza kwa kufanya vizuri huku akiwataka watu wengine kwenda kujifunza katika halmashauri hiyo.

.

Aidha ameongeza kuwa Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais  Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania  wajulikane wanakaa wapi kwani jambo la kuweka namba katika mitaa, barabara na nyumba katika Halmashauri ni jambo muhimu kwa kila mtanzania.

.