Dodoma FM

Wakazi wa Chididimo waiomba halmashauri kuwashirikisha katika suala la ununuzi wa mashamba yao

26 May 2022, 11:43 am

Na;Mindi Joseph.

Wananchi wa Mtaa Chididimo Kata Zuzu wameiomba  halmashauri ya jiji la Dodoma kuwashirikisha kikamilifu katika suala la kutaka kununua mashamaba yao kwa ajili ya kufanya kilimo cha kisasa cha zao la zabibu.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza  mbele ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Jabiri Shekimweri ambapo wamesema suala la kutaka kununua mashamaba yao bado lina ukakasi kwao.

.

Mkuu wa wilaya Mh. Jabiri Shekimweri Baada ya kusikia malalamiko hayo pamoja na maoni  ya wananchi wa Mtaa wa huo ametoa ushauri kwa halmashauri ya jiji la Dodoma ya nini cha kufanya ili kumaliza suala hilo.

.

Na Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya Mh. Jabir Shekimweri ametumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi hao juu ya suala la kutunza mazao yao waliyovuna kutokana na uchache wa mvua ya mwaka huu ili kujihadhari na tatizo la njaa.