Dodoma FM

Wanawake Ilazo waiomba serikali kuwapatia elimu ya mikopo

21 April 2022, 10:22 am

Na; Shani Nicolous.

Wanawake wa mtaa wa Ilazo jijini hapa wameiomba serikali na taasisi za mikopo kutoa elimu juu ya matumizi sahii ya mikopo hiyo.

Wakizungumza na Taswira ya habari wanawake hao wamesema kuwa mikopo huenda inatolewa lakini mwitikio ni mdogo kutokanana na ukosefu wa elimu juu ya namna bora ya kuitumia.

Wamesema viongozi wa mitaa kwa kutumia mikutano mbalimbali wawaelimishe wanawake hao ili kuepukana na changamoto  baada ya kupata mikopo hiyo na kushindwa kuirejesha.

.

Wamesema kuwa baada ya kutoa elimu na mikopo ni vema kuendelea kuwatembelea wananawake  na kujua mikopo hiyo inatumikaje na namna vikundi vinavyoendelea baada ya kupata mikopo na si kukaa ofisini.

.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Moses Mazengo ametoa wito kwa wanawake kuuunda vikundi ili kuwawezesha kupata mikopo hiyo kwani mashariti ya mikopo hiyo pamoja na kikundi kuwa na watu kuanzia watano na hairuhusiwi mmoja kupewa mikopo isipokuwa watu wenye ulemavu.

.

Haya yanajri baada ya baadhi ya wanawake wa mtaa huo kupatiwa mikopo ya halmashauri ambayo inawasaidia kufanya shughuli mbalimbali huku wengine wakidai hawana taarifa juu ya mikopo hiyo.